Rais wa Marekani, Donald Trump, anaripotiwa kusaini amri ya kuahirisha tena kuanzishwa kwa ushuru mkubwa wa bidhaa za China Jumatatu, masaa machache kabla ya mkataba wa biashara kati ya Washington na Beijing kumalizika.
Kusimamishwa kwa ushuru huo wa juu kutakuwa kwa siku 90 zaidi, kulingana na ripoti za Wall Street Journal na CNBC, zikirejelea viongozi wa serikali ya Trump. Ikulu ya White House haijajibu maswali kuhusu suala hilo.
Wakati Marekani na China zimekuwa zikipandisha ushuru kwa bidhaa za kila mmoja mwaka huu, huku viwango vikifika asilimia kubwa na kusababisha misukosuko katika biashara, nchi zote mbili mnamo Mei zilikubali kupunguza kwa muda.
Lakini mkataba wao wa kusimamisha viwango vya juu vya ushuru kwa siku 90 ulitarajiwa kumalizika Jumanne.

Post a Comment