Mwanamume aliyechukua nyoka wake na kumpeleka kuota jua katika bustani ya eneo ya umma amezua mjadala mtandaoni kuhusu wanyama wanaokubalika na wasiokubalika - katika maeneo ya umma.
Kundi la Friends of Barshaw Park lilisema lilipigiwa simu na watu ambao walikuwa na wasiwasi kuhusu mtu aliyepeleka hadi nyoka 20 kwenye bustani ya Paisley.
Ilimtaka yeyote atakayewaona nyoka hao kupiga simu polisi.
Mbali na kuwa na hofu, wenyeji wengi wamemtetea mmiliki wa nyoka - ambaye anaonekana kuwa mgeni wa kawaida eneo hilo.
Walisema hakusababisha madhara yoyote na pia aliwadhibiti nyoka wake wakati wote, na kuhoji ni kwa nini polisi wangehusishwa.
Picha za mwanamume huyo zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinamuonyesha akiwa mwenye furaha aliyepiga na nyoka wake huku wakiwa wamezunguka shingoni mwake au kusimama karibu naye na kutembea taratibu kwenye nyasi kufurahia jua.

Post a Comment