#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

Milioni 300 kuwezesha wananchi Karatu

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dkt. Lameck Karanga amekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 300 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalumu katika hafla iliyofanyika wilayani humo. Fedha hizo ni mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kwa lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji na biashara.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Dkt. Karanga amesema serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vinavyokidhi vigezo. Amesisitiza wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa maendeleo yao binafsi na jamii kwa ujumla.
Aidha, amevitaka vikundi vilivyopokea mikopo hiyo kuhakikisha vinarejesha fedha kwa wakati ili kutoa nafasi kwa vikundi vingine kunufaika na mpango huo.
Pia amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Chini ya Mkurugenzi Juma Hokororo kwa kuendelea kutenga na kusimamia vizuri fedha za mikopo kwa makundi maalumu kwa mujibu wa maelekezo ya serikali.
Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru serikali kwa kuwapatia mtaji utakaowasaidia kupanua shughuli zao za kiuchumi na kuongeza kipato cha familia zao.


Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv