Mabaki ya binadamu yanaaminika kupatikana ndani ya mabaki ya nyambizi Titan, Jeshi la Walinzi wa Pwani la Marekani linasema.
Vipande kutoka kwa nyambizi hiyo ndogo, ambayo ilizama kwenye eneo kulikotokea ajali ya Titanic, vilitolewa huko St John's, Canada, Jumatano.
Maafisa wanasema fremu ya kutua na kifuniko cha nyuma ni kati ya vifusi vilivyopatikana.
Wataalamu wa matibabu wa Marekani watafanya uchambuzi rasmi wa mabaki yanayodhaniwa, walinzi wa pwani walisema katika taarifa.

Post a Comment