Manchester City wanafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua beki wa kulia wa Paris St-Germain Achraf Hakimi, 24, na "haitasita" kulipa ada kubwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco. (Marca - kwa Kihispania)
Manchester United inaangazia kumsajili mcehezaji mwingine wa safu ya kati, huku mchezaji wa kimataifa wa Ecuador wa Brighton & Hove Albion Moises Caicedo, 21, akiongoza orodha yao, baada ya kushindwa kupiga hatua katika majaribio yao ya kumsajili Mason Mount. (Sunday- usajili unahitajika)
United haijaifurahia Chelsea baada ya habari za ofa zao kushindwa kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Mount, 24, kuvuja kwenye magazeti ya kitaifa. (Manchester Evening News)
Liverpool, Manchester United na Chelsea watafanya mikutano na maajenti wa mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, wiki ijayo kuhusu uwezekano wa kuhamia Ligi ya Premia. (Express)
Meneja wa Bayern Munich Thomas Tuchel ameiomba klabu hiyo kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 26, baada ya kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili Muingereza Declan Rice, 24, kutoka West Ham.. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)
Vilabu vitatu vya Premier League vinamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Eddie Nketiah, 24, huku The Gunners wakikaribia kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Kai Havertz, 24, wa Ujerumani (Mirror)
Brighton wamemtambua mshambuliaji wa Ajax Mohammed Kudus, 22, kama mlengwa wao mkuu msimu huu baada ya Mghana huyo kukataa kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Eredivisie(Mail)
Kiungo wa kati wa Feyenoord kutoka Slovakia David Hancko, 25, ameivutia Newcastle United ambao wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi (Mail)
Callum Hudson-Odoi yuko tayari kwa mazungumzo na Chelsea, huku vilabu vingi vya Premier League vikimfuatilia winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22. (Express)
Everton wana nia ya kumleta winga wa Leeds United wa Italia Wilfried Gnonto, 19, Goodison Park msimu huu wa joto(Football Italia)
Tottenham wamemtaja mlinzi wa Wolfsburg Mholanzi Micky van de Ven, 22, kwenye orodha ya wachezaji wanaowania nafasi ya ulinzi ambayo pia inamjumuisha beki wa kati wa Bayer Leverkusen wa Burkino Faso Edmond Taspoba, 24 (Mail)
Southampton wanatazamia kumsajili beki wa zamani wa Chelsea Derrick Abu, 19, kwa uhamisho wa bila malipo. (Mail)
Klabu ya Roma ya Serie A iko kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili beki wa Leeds United Rasmus Kristensen, 25, huku meneja Jose Mourinho akimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark. (Mail)
Manchester United inamfuatilia mlinda lango wa Serbia Djordje Petrovic, 23, ambaye alishinda tuzo ya uokoaji bora wa mwaka MLS msimu uliopita akichezea New England Revolution. (Manchester Evening News)
Sheffield United iko tayari kumuuza mshambuliaji wa Senegal Iliman Ndiaye, 23, kwa timu ya Everton inayoshiriki Ligi ya Premia msimu huu. (Football Insider)




Post a Comment