Pichani ni Mwanafunzi Ester Noah Mwanyilu
Jeshi la Polisi limetangaza kwenye gazeti la Serikali kuhusu kupotea kwa Mwanafunzi wa Kidato cha Tano Easter Noah wa Shule ya Sekondari Panda Hill. Pia kwa kupitia mfumo wa cyber crime kupitia namba aliyokuwa akiwasiliana nayo ya rafiki yake aitwaye Condoleza Robert. Pia inadaiwa Mwanafunzi huyo alipokuwa Kidato cha nne alishawahi kutoroka nyumbani kwenda kulala kwa mwanaume.
Uchunguzi bado unaendelea ili kujua nini kimemkuta Mwanafunzi huyo. Tumewahoji walimu, wanafunzi na taratibu za kitaalamu za kichunguzi zinaendelea.
Marafiki zake walikuwa wakisema Easter alikuwa akilia (hapo shuleni kuna sehemu huwa wanafunga kinanda kwa ajili ya uimbaji) na walijua kuwa alikuwa kwenye maombi kumbe alikuwa analia na baada ya hapo hakuonekana tena. Pengine kile kitendo cha kuangalizia mtihani na alisemwa na pengine ikampelekea kufanya kitendo kisichokuwa sahihi"
Jalada la uchunguzi limeshafunguliwa tangu tarehe 18, May, 2023. Baada ya taarifa hii Jeshi la Polisi walifuatilia alibainika kuwa ametoroka shuleni na kutokomea kusikojulikana .Uongozi wa shule ulijulisha wazazi wa Mwanafunzi huyo.
Jitihada mbalimbali zilifanyika ikiwa na pamoja na kuwahoji walimu wa shule, wanafunzi, Marafiki wa Ester na jumbe zote alizokuwa akiandika zilizoachwa na Mwanafunzi huyo zimechukuliwa na kupelekwa kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini kama ni jumbe za mwanafunzi huyo aliandika mwenyewe au la"
Pia ni vyema kama kuna mtu yupo naye Mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Easter Noah wa Shule ya Sekondari Pandahili aliyepotea 18, May, 2023 ni vyema akamuachia au kama yupo sehemu yoyote tujue kwa sababu hayo ni maumivu makubwa, chukulia Mtoto wako amepotea na hajulikani alipo utajisikiaje? Fikiria Sisi kama ni wazazi tunajisikia maumivu sana. Na Leo tutakuwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa ili kujua tumefika hatua gani.
Pia tutawasilisha taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alitoa maagizo kwamba huyu Mwanafunzi atafutwe ili ajulikane alipo. Na alinipigia na kunitumia meseji kwamba baada ya taarifa kukamilika nimtumie taarifa ofisini kwake"
Post a Comment