#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

KIRIA AWAZAWADIA MILIONI 2 WALIMU NAISINYAI KWA UFAULU

MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Kiria Ormemei Laizer amewapongeza walimu wa shule ya sekondari Naisinyai kwa kuwapatia zawadi ya kitita cha shilingi milioni 2 baada ya wanafunzi 33 wa kidato cha sita wa shule hiyo kufaulu mtihani wao na kuchaguliwa kujiunga na  vyuo vikuu. 

Na Mwandishi wetu, Simanjiro 

Pia, Diwani wa Kata ya Mirerani, Salome Nelson Mnyawi, pia amewakabidhi walimu wa shule hiyo sh300,000 ili kumuunga mkono Kiria katika kuwapongeza walimu hao.

Kiria amesema amejitolea Sh2 milioni kwa walimu hao ili wakanywe soda za pongezi kutokana na ufaulu mzuri wa wanafunzi wa kidato cha sita wa shule hiyo.

"Najua shule ya sekondari Naisinyai imefaulisha vyema wanafunzi wa kidato cha sita, hivyo fedha hizo zitachangia furaha yangu kwa walimu kutokana na ufaulu huo mzuri," amesema Kiria 

Mkuu wa shule ya sekondari Naisinyai, William Ombay amesema wanafunzi 33 wa shule hiyo walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha sita na wote wamefaulu kwenda chuo kikuu.

"Kati ya wanafunzi hao 33, watatu wamepata daraja la kwanza, 27 daraja la pili na watatu daraja la tatu, hivyo hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la nne wala sifuri," amesema mwalimu Ombay.

Diwani wa kata ya Naisinyai, Taiko Kurian Laizer amewapongeza walimu hao kwani wanafunzi wasingefaulu ingekuwa lawama kwao ila hivi sasa pongezi ni za watu wote.


"Kwenye kufanya vizuri tunakuwa tunapata sifa wote pamoja ndiyo sababu hata mimi nimepongezwa kwenye magurupu ya Whatsapp ila wanafunzi wangefeli ingekuwa aibu yenu walimu," amesema Taiko.

Diwani wa kata ya Mirerani, Salome Mnyawi amemuunga mkono Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya kwa kuwapongeza walimu hao kwa kuwapatia Sh300,000 kwa kufanikisha ufaulu huo.

"Hii natoa changamoto kwa walimu wa shule yangu ya sekondari Tanzanite iliyopo kata ya Mirerani kuhakikisha wanaendelea kufundisha vyema ili wanafunzi wafaulu nao tuwazawadie," amesema Salome.

Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Mosses Makeseni amesema wanafunzi hao wamefaulu vyema, ingawa ndiyo mara ya kwanza wanafunzi wa Naisinyai kufanya mtihani wa kidato cha sita.

Mwenyekiti wa kijiji cha Naisinyai, Merika Makeseni amesema walimu wanastahili kupongezwa kutokana na matokeo hayo kwani wao ndiyo wanaowafundisha wanafunzi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv