1 Na popote ukiwepo
Usiwe kama libopo
Usijione simpo
2 Yalo yako ujikite
Mitihani uipite
Hadi ukate upete
3 Usisikie uzushi
Uyafanye kwa utashi
Usiwe na nukusani
4 Tembea nenda na Mungu
Atoae kwa mafungu
Ajua wako uchungu
5 Na hawana utu watu
Mpaka uwape kitu
Nnasi hawana sukutu
6 Kunayo leo na kesho
Lazima litoke jasho
Achana nayo mipasho
Abuuabdillah ✍️
0744883353
.jpeg)
Post a Comment