#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

Serikali kuunganisha Leseni za Biashara zinazotolewa na BRELA na Halmashauri kuwa moja

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali iko mbioni kuunganisha leseni  ya biashara inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Halmashauri kuwa leseni moja ya biashara itakayowawezesha kufanya biashara Nchi nzima.

Dkt Kijaji ameyasema hayo Agosti 17, 2023 wakati akijadiliana kuhusu maendeleo ya biashara na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa  Ofisi za Mkuu wa Mkoa ikiwa ni mwendelezo wa mikutano hiyo katika kila mkoa ambapo Dodoma ni Mkoa wa Saba baada ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Morogoro Mbeya na Songwe.

Aidha, Dkt. Kijaji  amewashauri wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma kusajiri biashara zao, kuwa waaminifu katika kurudisha mikopo na kuchangamkia fursa za biashara kwa kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi pamoja na fursa za kibiashara katika masoko ya EAC, SADC, AGOA  na AfCFTA yenye soko lenye jumla ya watu bilioni 1.3. bila kutozwa kodi wala ushuru wowote.

Dkt. Kijaji pia amesema Wizara yake inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji  nchini (MKUMBI) ambapo hadi sasa imefuta au kupunguza Tozo, Ada na Faini 374 kati ya 380  na katika kipindi cha 2023/24  Tozo, Ada na Faini 67zimefutwa au kupunguzwa.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe akijibu Baadhi ya changamoto za wafanyabiashara hao amesema Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi na itaendelea kuishirikisha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini pamoja na jitihada za uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini.

Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti  wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo  Mhe Fransis Mtinga aliwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa Kamati hiyo iko tayari kushughulikia  changamoto zote za kisheria na sheria ndogo zinazowakabili katika ufanyaji biashara.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Rosemary Senyamule amemhakikishia Waziri Kijaji kuwa Mkoa wake kwa kishirikiana na wadau mbalimbali utashughulikia changamoto zote ziliowasilishwa na wafanyabiaahara hao ikiwemo utoaji wa mafunzo kwa wajasiliamali na kuanzisha kituo cha huduma za pamoja za kuhudumia wafanyabiashara.

Awali Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma Bw Hamis Fungameza  pamoja na wafanyabiashara wengine walipata fursa za kuwasilisha changamoto mbalimbali ikkwemo  upatikanaji wa Mitaji, Mikopo yenye masharti magumu,  masoko ya mazao, kodi ambazo si rafiki , miundombonu ya barabara na masoko hafifu


Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv