Nyumba sita zimesombwa na Mto Naranjo uliovimba katika Jiji la Guatemala, huku watoto tisa wakiwa miongoni mwa waliotoweka.
Takriban watu sita wamefariki na wengine 12 hawajulikani walipo baada ya mto uliojaa maji kusomba nyumba katika mji mkuu wa Guatemala.
Mapema Jumatatu, maji kutoka Mto Naranjo yalitiririka kupitia mtaa wa mabanda katika Jiji la Guatemala uitwao Dios es Fiel, au Mungu ni Mwaminifu, na kuharibu angalau nyumba sita zilizokuwa zimejengwa chini ya daraja, kulingana na shirika la Kitaifa la Uratibu wa Kupunguza Majanga la Guatemala (CONRED). )

Post a Comment