#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

Mchina Aliyejifungua Tanzania Asifia Huduma Nzuri hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam


Raia wa China, Liya Zhang (31), ambaye amejifungua watoto mapacha watatu wa kiume katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam ameshukuru kwa huduma nzuri alizopata.


Raia huyo alijifungua watoto hao siku ya Jumapili usiku hospitalini hapo na mpaka sasa anaendelea vizuri yeye na watoto wake hao watatu.

Akizungumza hospitalini hapo, Liya alisema awali wakati anahudhuria kliniki alidhani kuwa ana ujauzito wa mtoto mmoja lakini baada ya vipimo alishtuka kuambiwa kuwa ana watoto wa tatu.

“Nawashukuru sana madaktari bingwa wa watoto, Dk. Rahim na Dk. Supriya Khan kwa namna walivyonihudumia tangu awali mpaka najifungua, nimepata huduma nzuri sana hapa Regency na watoto wangu kama unavyowaona wako vizuri kabisa,” alisema Liya kwa lugha ya Kiswahili fasaha.

Liya alisema si mara yake ya kwanza kujifungua hospitalini hapo kwani mwaka 2009 alijifungua mtoto wa kwanza wa kike hospitalini hapo na baadaye alikuja kujifungua mengine wawili wa kiume pia hospitaini hapo hapo na sasa amefurahi kupata watoto wa kiume watatu.

“Nilipata mtoto mmoja wa kike mwaka 2009 na baadaye nikapata mapacha wawili wa kiume na juzi Jumapili nimepata mapacha watatu kwa hiyo sasa nina jumla ya watoto sita na wote nimejifungua katika hospitali hii hii ya Regency na nadhani nitakuwa nimemaliza kwa kweli inatosha,” alisema Liya huku akicheka kwa nguvu.

Daktari bingwa wa watoto wa Regency, Dk. Rahim alisema wamekuwa wakimhudumia Liya tangu uzao wake wa kwanza ambapo alipata mtoto wakike hospitalini hapo na ujauzito wa pili ambapo alifanikiwa kupata watoto wa kiume mapacha.

“Na huu ni ujauzito wake wa mara ya tatu ambapo amefanikiwa kupata mapacha watatu wote wa kiume na uziri ni kwamba anaimani nasisi kwa muda mrefu kwani kila anapotaka kujifungua amekuwa akija hapa Regency na tunashukuru watoto wake wote wanaendelea vizuri sana,” alisema

“Tumekuwa tukihudumia wanawake wengi sana wanaojifungua lakini hii ni mara ya kwanza hapa Regency kuhudumia mwanamke kupata watoto watatu, hii ni habari njema kwetu sote,” alisema

CHANZO: GlobalTvOnline

Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv