Kwa uchache, Dr. Gwajima ametolea mfano wa Mtengeneza maudhui mmoja ambaye hivi karibuni ameonekana akisambaza maudhui ya kuuza figo za Mtoto, mwingine akionesha maudhui ya kuandaa vinywaji na vyakula vichafu na kujitapa kuwa anawauzia Wananchi wa Kariakoo na wa maeneo mengine.
Maudhui mengine yaliyokemewa na Waziri Gwajima ni ya wale wanaosambaza maudhui ya kufanya mapenzi hadharani yakiwemo ya jinsia moja, wengine wakisambaza maudhui kuhusu fursa za kujipatia fedha kwa njia zisizoeleweka.
Waziri Gwajima amewataka Watengeneza maudhui kuzingatia weledi na miongozo yote na kama Mtu hana elimu na ufahamu kuhusu kuandaa maudhui ya mtandaoni aache mara moja kwakuwa ataharibu na atawajibishwa ambapo amewataka wale wote ambao wamepakia maudhui kinyume na miongozo husika wayafute haraka maudhui hayo mtandaon

Post a Comment