Mshambulizi wa Manchester City Haaland anatafuta ushindi wa tatu mfululizo katika mbio za Kiatu cha Dhahabu cha Premier League msimu huu.
Hilo ni jambo ambalo hapo awali limefikiwa na Alan Shearer na Thierry Henry, ambao ni washambuliaji wawili wazuri zaidi kuwahi kucheza katika ligi ya daraja la kwanza England.
Haaland anatazamia kuwa mfungaji bora wa Premier League tena baada ya kushinda Kiatu cha Dhahabu kwa tofauti ya mabao matano msimu wa 2023/24, wakati kiungo mshambuliaji wa Chelsea Cole Palmer alipoibuka kuwa mpinzani wake wa karibu zaidi.
Nyota wa Man City, Haaland alifunga mabao 27 msimu uliopita na kupiga hat-trick mbili, ikiwa ni pamoja na mabao manne kwa moja katika ushindi dhidi ya Wolves kuelekea mwisho wa mwaka. Ushujaa wake uliisaidia timu ya Pep Guardiola kushinda taji la kihistoria la nne mfululizo la Premier League.

Post a Comment