Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limepokea magari mapya mawili aina ya Robur Armored TLC 300 ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha utendaji wa kazi za kila siku.
Magari hayo yamepokelewa leo Oktoba 23, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justin Masejo na kuyakabidhi kwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoani humo kwa ajili ya kuanza kutumika.
Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wanaendelea kufanya maboresho ya kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ya usafiri na kuahidi kuwa watahakikisha magari hayo yanatunzwa vyema.
Post a Comment