Kupitia ukurasa wake wa Facebook Mwaimbaji wa Nyimbo za Injili nchini Tanzania Sylvia Mwangunga ameandika ''Walio shinda hawakukata tamaa pindi walipo anza ilikiwa ni ngumu kushinda sababu safari yao haikuwa rahisi walishinda kwa kuwa hawakutishika wala kuogopa vitisho vilivyo mbele yao waliomba Mungu nae akawashindia''
Maneno haya ya Sylvia Mwangunga ameyaandika kwa msisitizo mkubwa ikiwa ni kuwapa moyo na matumaini kwa wale walianza kufanya jambo fulani lakini wanapitia kipindi ambacho wanahitajika kutokuta tamaa ya kuendeleza jambo hilo. Ukimbuke kuwa muda mwingi watu hupitia mambo mengi yenye kukatisha tamaa hasa changamoto mbalimbali za kimaisha

Post a Comment