Wanafunzi wa shule ya msingi Emishiye iliyopo kijiji cha Losoito Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wataondokana na changamoto ya msongamano madarasani baada ya wadau wa elimu Ako Tanzania Community Support kuwajengea madarasa manne.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Losoito wamelishukuru shirika lisilo la kiserikali la Ako Tanzania Community Support kwa kuwajengea madarasa manne ya shule hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Losoito, Samson Sakwei na mkazi wa kijiji cha Losoito, Tipiliti Kuya wameeleza kwamba Ako Tanzania imekuwa msaada mkubwa kwao.
Mwalimu mkuu shule ya msingi Emishiye, Loishiye Laizer amewashukuru Ako Tanzania Community support kwa kusaidia shule hiyo.
Mkurugenzi wa shirika la Ako Tanzania Community support, Hilda Kimathi ameeleza kwamba wamesaidia jamii ya eneo hilo kwa kujenga madarasa, kumalizia zahanati na mradi wa lishe wa kilimo cha mbogamboga.
Post a Comment