Mtangazaji maarufu nchini Kenya Betty Kyallo na mpenzi wake Charlie Lemmy wametangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja!
Wapenzi hao walikua kwenye mitandao yao ya kijamii kutangaza habari njema hiyo na kuweka picha husika.
Betty Kyallo aliangaza akiwa amevalia rangi ya zambarau akionyesha tumbo lake linalokua wakati Charlie akiwa amesimama upande wake.
Betty Kyallo aliweka picha hiyo na akaandika:
"Tumekua tukipika kitu tamu sana. Mungu ndiye mkuu zaidi."
Wafuasi wao hawakuweza kukaa kimya wakajaza sehemu ya maoni kwa ujumbe wa pongezi.
Dada yake Betty Kyallo Gloria Kyallo alitoa maoni kwa alama za upendo.
Mulamwah aliandika:
"Hongera Betty"


Post a Comment