#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

Shirika lisilo la kiserikali la SOS Children's Villages tawi la Karatu limekabidhi pikipiki saba kwa vikundi vya vijana wilayani humo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kiuchumi na kuwainua kimaisha.

Pikipiki hizo zimekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Ndg. Juma Hokororo, katika hafla iliyofanyika wilayani Karatu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Hokororo amelipongeza shirika hilo kwa hatua hiyo muhimu ya kuwekeza kwa vijana, akieleza kuwa uwezeshaji huo utasaidia kuongeza ajira na kipato kwa wanufaika pamoja na familia zao.
Amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu, hasa kwa makundi ya vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.
Aidha, amemshukuru Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuimarisha mazingira rafiki ya ushirikiano kati ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali, ushirikiano huo umewezesha mashirika mengi kukua na kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa na wa mtu mmoja mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, pikipiki hizo saba zimegharimu zaidi ya shilingi milioni 19, na zinatarajiwa kusaidia vijana hao katika shughuli za usafirishaji na biashara ndogo ndogo, hivyo kuongeza fursa za ajira na kipato katika jamii ya Karatu.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv