Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameshiriki mdahalo wa hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Ahadi za Nchi kwenye Jukwaa la kizazi chenye usawa.Katika Mjadala Mhe. Dkt. Gwajima amebainisha maeneo makuu ya vipaumbele, ili kutekeleza ahadi hizo ikiwa ni pamoja na kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi, Ushiriki wa Wanawake katika kufanya maamuzi, na uingizaji wa Jinsia katika Sera za Kisekta.
Aidha, ameelezea jinsi gani Tanzania inaendelea kuhakikisha wanawake wanainuliwa kiuchumi ambapo, imehamasisha na kuratibu kuundwa kwa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kuanzia ngazi ya taifa, mikoa, wilaya na hadi kata na vijiji.


Post a Comment