Abiria wanaotumia usafiri wa Daladala kuingia katikati ya Mji wamelazimika kutumia usafiri mbadala ikiwemo Guta, Bodaboda na Magari ya Mizigo kutokana na mgomo huo ulioanza leo Jumatatu Agosti 14, 2023 sababu ikitajwa ni Bajaji kuingilia huduma ya kusafirisha abiria kama wanavyofanya Daladala
Huo ni mgomo wa pili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na nusu, ambapo baadhi ya madereva Daladala wamedai Mamlaka za Jiji la #Arusha zimeshindwa kufikia muafaka kuhusu mvutano huo wa Bajaji na Daladala

Post a Comment