1 Mpole, mcheshi sana, mtii mwenye huruma
Kamjalia rabbana, kuhitimu kuwa mama
Hapendi yaso maana, huchunga asije zama
Kwenye wengi wasichana, Neema hana mfano
2 Ni mpishi na twabibu, si mja wa ujivuni
Nimemfanya swahibu, awe pangu ubavuni
Namuona kama dubu , na siyo katika kuvu
Ukipenda ita Grace,namuombea mazuri
3 Shingo yake yanikosha, jinsi ilivyopangika
Ana ngozi ya kitasha , na mwili umemwagika
Bila mboga ashibisha, pishi lake uhakika
Aenda kama haendi, kumbe ndio mwendo wake
4 Usafi ni jadi yake, vazi lake la kipwani
Bado angali mteke, yuko mbali na uhuni
Sitaki awe mpweke, furaha iwe pomoni
Neema binti Chaula, Mola akupe sakina
Abuuabdillah ✍️🇹🇿

Post a Comment