Mapinduzi ya Gabon na Niger ni ya hivi punde zaidi katika kile kinachoonekana kuwa mwelekeo unaoongezeka wa uingiliaji kati wa kijeshi katika Afrika Magharibi na Kati.
Mwaka jana yalikuwa matano. Matatu yaliishia bila kuwa na mafanikio (Guinea-Bissau, Gambia na taifa la kisiwa la São Tomé na PrÃncipe) na mawilii, yote nchini Burkina Faso, yalifanikiwa.
Mnamo 2021, kulikuwa na majaribio sita ya mapinduzi barani Afrika, manne kati yao yalifanikiwa.
Lakini kuenea kwa uvamizi wa kijeshi bado ni chini sana kuliko miaka iliyofuata baada ya uhuru.
Kwa ujumla, Afrika imekumbwa na mapinduzi mengi kuliko bara lolote lile. Kati ya mapinduzi 18 yaliyorekodiwa ulimwenguni tangu 2017, yote isipokuwa moja - Myanmar mnamo 2021 - yamekuwa barani Afrika.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat mwaka jana alielezea wasiwasi wake kuhusu "kuzuka upya kwa mabadiliko ya serikali kinyume na katiba".
.jpeg)
Post a Comment