Woga ni moja kati ya maadui wa kubwa wa maendeleo ya mtu binafsi. Unaweza kutafuta watu wa kuwalaumu kwenye maisha yako lakini amini kuwa maisha ni yako na sehemu kubwa ya matatizo yanayo kukuta ni wewe mwenyewe ndio chanzo za matatizo hayo kwa kuogopa kutatua matatizo yako binafsi.
Kwanza unatakiwa kujua woga ni moja kati ya muuaji namba moja duniani wa ndoto na malengo ya binadamu katika kufanikiwa maisha hii ni kutokana na kauli za madaktari kuwa woga ndio unachangia wagonjwa wengi kupoteza matumaini na maisha kutokana na woga wa matatizo waliyonayo ‘’ waoga hufa mapema kuliko wasio na woga’’ hii ni ishara tosha kabisa kuwa woga ni hatari sana kwa maisha ya binadamu.
Sasa ni miaka mitatu tangu nilipogundua adui yangu mkubwa ni uwoga na kuanza kupambana nae na matokeo nayaona kwenye maisha yangu kama ukiweza kwenda na mimi mwazno hadi mwisho wa somo hili basi utapata ushujaa na kuweza kupambana na woga na kuwa jasiri kwenye kila kitu unacho kifanya mimi kabla sijagundua adui huyu nilipata shida sana kwenye uchumi, muonekano, mafanikio hadi kwenye mahusiano yangu kila kitu kilianguka na kuaribika hii ni uwoga tuu ulifanya haya kwenye maisha niliyokuwa naishi.
Lakini nikupe tuu taadhari kuwa woga hautakiwi kuukwepa bali kuuvaa na kupambana nao maana woga unanjia nyingi na mipando ya kukufanya ukate tamaa na kujikwamisha mwenyewe kwenye maendeleo na mambo mengine unachotakiwa kukifanya ni kuamini kuwa utashinda na kufanikiwa na kukubali kuwa haujashindwa bali ni woga tuu ndio unakusumbua
Kwanini uache woga ukunyanganye mahusiano yako, Uchumi wako na kukuvujruga kabisa nikikumbuka mimi kabla sijakuwa shujaa nilipitia wakati mgumu sana biashara ilikufa mahusiano yaliaribika kodi iligeuka deni na kweli nilinyeshewa na mvua ya madeni huku kila nilipo tafuta njia mbeleyangu nilikutana na woga tena woga ukamkaribisha ndugu yake wasiwasi nakumbuka kuna kipindi hali ilikuwa mbaya hadi kufikia hatua ya kula kipande kimoja cha muogo kwa siku na siku nyingine bila ya kula kitu kabisa mke alirudi kwao na marafiki wote walikimbia kweli woga ulikuwa umeniweza.
Nakumbuka vuzuri kabisa nilishindwa maisha hadi nikarudi nyumbani kwa wazazi lakini bado woga haukuniacha ukanifata hadi huko na kunishambulia mpaka siku nilipo kuja kugundua adui aliyekuwa nadni yangu sina ujanja na siwezi kumkimbia zaid ya kupambana nae nah ii ndio siku nilianza hatua ya kwanza ya mafanikio yangu.

Post a Comment