Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi Stella Ludman Maliti na Zacharia Mataiga Mwita wanaoendelea na masomo ya sekondari, miongoni mwa washiriki na washindi wa shindano la Hisabati Afrika la Pan African Mathematics Olympiads (PAMO 2024), lililofanyika chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
TCRA inaamini kuwa hisabati kama mojawapo ya masomo ya sayansi ni msingi mkuu katika ujenzi wa uchumi wa kidijiti unaotegemea TEHAMA. Shime kwa wanafunzi na vijana kujikita katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) ili kupata fursa ya kushiriki maendeleo ya Dunia katika zama za kidijiti.

Post a Comment