Huko nchini Somalia wataalamu wa uteguzi wa Mabomu wapokwenye hofu juu ya kazi yao baada ya kuibuka kwa wimbi kubwa la utegwaji wa mabomu hasa katika maeneo ya uma.
Akiwa amevalia suti kubwa ya kujikinga na kofia ya chuma, Mohamed Ahmed kuelekea lori ambapo vilipuzi vilivyowekwa kwenye simu vimetegwa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Kwa bahati nzuri kwa Ahmed, afisa wa polisi, hili ni zoezi la mafunzo na kifaa ni dummy.
Mashambulio ya mabomu kwa kutumia mbinu hii, au mashambulizi ya kujitoa mhanga kwa magari, ni jambo la kawaida nchini Somalia, ambapo waasi wanaohusishwa na al Qaeda wamekuwa wakipigana na serikali tangu 2007.

Post a Comment