Huduma ya mabasi kwa abiri wanaoshuka katika Train ya SGR kwa mikoa ya Dodoma Na Morogoro inaendelea na kazi ya kutoa huduma hiyo katika kipindi hiki cha sikukuu huku wakiednelea na msimamo wao uleule wa huduma bora kwa gharama nafuu wakati mabasi mengine yakiongeza gharama ya nauli kwa safari lakini Faima Shuttle Bus Service haitapandisha nauli kwakuwa inawajali watanzania na kutambua umuhumu wa safari kipindi hiki.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasafiri na watumiaji huduma ya Faima wemewaeleza waandishi wetu kuwa hii imekuwa suluhisho la matatizo ya usafiri hasa kipindi cha mwisho wa mwaka, ''Kutoka hapa SGR mpaka Mtumba ilikuwa inanigharimu sana lakini pia sikuwa na uhakika wa usafiri lakini kwa sasa hawa Faima wamekuwa kimbilio letu na ukiangalia hata nauli yao ni nafuu kwa kweli kwa 5,000/= tuu naweza kufika nyumbani salama'' Alitueleza moja wa abiri mkoani Dodoma.
Tangu kuanza kwa huduma ya Faima Shuttle Bus Service abiria wamekuwa na uhakika wa kuwahi safari zao huku wakihakikishiwa usalama wa mizigo yao pale wanapokuwa ndani ya Faima Shuttle Bus Service kwakua Faima inawahudumu wenye uaminifu na kazi yao huku madereva wakiwa na elimu ya uhakika na kukubalika kitaifa na kimataifa (Professional Drivers ) hivyo abiria anakuwa na amani wakati akiwa safarini.


Post a Comment