Abiria wanaosafiri na Treni ya SGR kutoka Dar es salaam kuelekea mikoa ya Morogoro na Dodoma wanaendelea kufurahia huduma ya Faima Shuttle Bus Service kwa kuepukana na changamoto ya Usafiri wa kufika katikati ya miji hukia lakini pia huduma hii inaguza viunga vya mji yote husika kwa wakati mmoja.
Tangu kuanza kwa kwa huduma hii wasafiri wamekuwa wakifurahia usafiri wa uhakika kutokana na upatikanaji wa mabasi ya Faima katika train station za Dodoma na Morogoro ambapo hapo awali kabla ya kuanza kwa huduma hii ilikuwa changamoto kubwa kwa wasafiri wanaposhuka katika treni, Kupitia shirika la reli Tanzania TRC kufungua mlango wa wawekezaji kuboresha utoaji wa huduma kwa watanzania basi changamoto hiyo imefikia kikomo.

Post a Comment