Zoezi la uapisho wa mawaziri wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha The Arusha East African Training Institute limefanyika jana, tarehe 30 Januari 2026, katika viwanja vya chuo hicho.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wabunge wa chuo, mawaziri, viongozi wastaafu, uongozi wa chuo pamoja na wanafunzi. Zoezi hilo lilifanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia taratibu za chuo.
Rais wa Chuo, Bw. Allen Ludovick Jeremiah, aliwaapisha mawaziri hao wapya na kutoa hotuba, akiwataka viongozi walioapishwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kwa maslahi ya wanafunzi wote.
Uongozi wa chuo umepongeza kukamilika kwa zoezi hilo na kuwatakia viongozi wapya kila la heri katika majukumu yao ya uongozi.
.jpeg)
Post a Comment