Mradi huo wa kipekee unatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa Arusha kwa kuunganisha uhifadhi wa mazingira, ufugaji wa nyuki na shughuli za utalii. Kupitia mradi huo, wageni wa ndani na nje ya nchi watapata fursa ya kujifunza kuhusu uzalishaji wa asali, umuhimu wa nyuki katika uhifadhi wa mazingira, pamoja na kushiriki uzoefu wa kiutalii unaohusisha mazingira asilia ya Jiji la Arusha.
Aidha, mradi huo unalenga:
• Kutoa ajira kwa vijana na wanawake
• Kuongeza kipato cha wafugaji wa nyuki
• Kuhamasisha uhifadhi wa mito na misitu
• Kuongeza mapato ya Jiji kupitia utalii wa kiikolojia (eco-tourism)
Bonde la Mto Naura na Mto Themi pamoja na Mlima Suye ni maeneo yenye mandhari ya kuvutia na umuhimu mkubwa wa kiikolojia, hivyo kuifanya Arusha kuendelea kujiimarisha kama kitovu cha utalii si tu wa wanyamapori bali pia utalii wa kiikolojia na kilimo.
Hatua hii inaonyesha dhamira ya Jiji la Arusha katika kubuni miradi bunifu ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi sambamba na kulinda mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho.


Post a Comment