Washiriki mbalimbali wa kikao kazi cha 6 cha Serikali Mtandao wametembelea banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupata elimu kuhusu utekelezaji wa majukumu yake na uelewa wa sekta ya mawasiliano.
Usa River Media0
Kikao hicho kinafanyika jijini Arusha kwa lengo la kuwakutanisha wadau wa TEHAMA na kujadili umuhimu wa matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji kazi wa serikali unaolenga kuleta maendeleo yenye tija.
Washiriki wameiopongeza TCRA kwa usimamizi madhubuti wa sekta ya mawasiliano, na kutoa rai ya kuendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii kuhusu matumizi sahihi na salama ya huduma na bidhaa za mawasiliano.
Post a Comment