Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Toba Alnason Nguvila ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani Jiji la Arusha (Bonden City Bus Terminal), Februari 14, 2026, ikiwa ni zaiara yake ya kwanza jiji la Arusha tangua kuanza kutumikia wadhifa huo wa Katibu Tawala katika mkoa wa Arusha.
Dkt. Nguvila ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo hasa kwa kuzingatia ilikuwa ni kilio cha muda mrefu cha wakazi wa Arusha kuwa na Stendi ya kisasa kwa kuwa stendi inayotumika sasa ina eneo dogo na kusababisha uwepo wa standi bubu kwenye makazi ya watu, zinazosababisha pia msongamano wa magari mjini na ndani ya makazi ya watu.
"Tunamshukuru Mhe.Rais Mama yetu mama Samia kwa kujenga stendi hii, stendi ambayo inakwenda kupandisha uchumi wa wananchi wa maeneo haya"Amesema Diwani wa Kata ya Muriet.
Mradi huo unatekelezwa na serikali ya awmu ya sita kwa gharama ya shilingi Bilioni 14.3 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia ikiwa ni sehemu ya miradi ya kimkakati katika majiji yote nchini.
Lengo la mradi huo ni kuboresha mazingira ya usafiri kwa abiria wanaoingia na kutoka katika Jiji la Arusha, ikiwa ni stendi ya kisasa yenye uwezo wa kutoanhudla zote muhimu kwa wasafiri kwa wakati.
Awali, kiasi hicho cha fedha kitajumuisha ujenzi wa jengo kuu la mabasi lenye ghorofa 1 zenye sehemu za kusubiria usafiri, maduka 23, maeneo mawili ya wafanya biashara za vyakula, vyoo vya kisasa, nyumba ya walinzi, vituo vya ukaguzi, vituo vya kukusanyia taka pamoja na sehemu ya kukutania wakati wa dharura.





Post a Comment