Mbunge wa Jimbo la Karatu, Mheshimiwa Daniel Awack, ameanza rasmi ziara ya siku 11 kuwashukuru wananchi kwa imani waliyoionesha kwake.
Akiwa Kata ya Kansay, ameahidi kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga kituo cha afya na tayari amenunua gari la kubebea wagonjwa (ambulance) ili kuboresha huduma kwa wananchi.
“Miaka mitano ijayo ni miaka ya tabasamu kwa Karatu,” – akiahidi maendeleo katika kata zote na kukamilisha miradi iliyobaki.
Wananchi wamepokea ziara hiyo kwa furaha, wakitoa shukrani na kuwasilisha changamoto zao kwa maendeleo ya pamoja.



Post a Comment