Asema ni utekelezaji wa ndoto za Rais Samia kutoa uhakika wa Matibabu kwa Watanzania Diwani Dogo Janja amshukuru Rais Samia kwa utekelezaji wa ahadi yake
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amezindua zoezi la utekelezaji wa uandikishaji wa Kaya 12,741 katika mfumo wa Bima ya afya kwa wote ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakianza na kaya maskini zinazotambuliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF.
Kwenye Ofisi ya Kata ya Ngarenaro Jijini Arusha leo Februari 03, 2026, Mhe. Makalla amesema kutekelezwa kwa Bima hiyo ni utekelezaji wa maono ya Rais Samia ambapo kwa Mkoa wa Arusha jumla ya walengwa 56,963 wanatarajiwa kunufaika na mpango huo wa awali wa Bima ya afya kwa wote.
“Naungana nanyi katika Kata hii kwenye siku hii muhimu katika mageuzi ndani ya nchi yetu ya Tanzania na ambazo ni ndoto za Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kama alivyotangaza kuwa ndani ya siku 100 ataanza na makundi maalumu na kaya zisizojiweza kuwa zinapata bima ya afya na ametekeleza na leo ni kiashirio kuwa ahadi yake tumeizindua leo kwa kugawa bima za afya.” Amesema Mhe. Makalla.
Kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Ngarenaro, Diwani wa Kata ya Ngarenaro Mhe. Abdulaziz Chande maarufu kama Dogo Janja, amemshukuru Rais Samia kwa utekelezaji wa ahadi yake hiyo, akisema Bima hiyo ya afya inaenda kuwa mkombozi na msaada kwa wananchi wengi ikiwemo wale wasiokuwa na uwezo wa kiuchumi wakiwemo wazee. cc: @amosmakalla @ofisi_ya_diwani_ngarenaro @baba_keagan @maxmillianiranqhe @kayombojohn











Post a Comment