Mkaguzi wa magari kutoka ofisi ya Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkaguzi wa Polisi Wafula Shedrack akiwa na Koplo Ramadhani wamewatahini madereva 64 wa udereva daraja C katika kufanya mafunzo kwa vitendo juu ya uendeshaji gari na kwa kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani.
Madereva hao kutoa Chuo Cha Veta Mkoani Pwani waliendesha Bus kutoka stendi ya mabasi Kibaha hadi Mbezi kwa dereva mmoja mmoja kuendesha umbali tofauti tofauti ili kubaini uelewa wao wa namna ya uendeshaji mabasi makubwa kwa vitendo, lengo likiwa ni kuzalisha madereva wenye sifa stahiki za kuendesha mabasi makubwa ya abiria kwa sifa na vigezo vilivyowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungo wa Tanzania kupitia Sheria ya Usalama Barabarani.



Post a Comment