#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

USIKU WA KIMATAIFA WA REHEMA (INOM) 2026 WAKARIBIA KWA SHANGWE


 

Kwa mara nyingine tena, wakati wa Pasaka unapokaribia, mioyo ya waumini inaelekezwa kwenye rehema za Mungu kupitia tamasha la kiroho linalongojelewa kwa hamu kubwa. Usiku Kimataifa wa Rehema (INOM) 2026 unatarajiwa kufanyika tena mwaka huu, ukiwa na lengo la kuleta wokovu, uponyaji na ukombozi kwa wengi.

Tukio hili kubwa la kiroho linaloandaliwa na Kanisa la Christ Mandate kupitia kiongozi wake, Dr. Malachi Joseph, litafanyika Ijumaa Kuu (Good Friday) katika eneo la Bunju B, Katavi Street – Christ Mandate City.

Nyota wa Muziki wa Injili Kukaribishwa

Usiku huu wa pekee utakuwa na burudani ya kiroho itakayotolewa na waimbaji mashuhuri wa injili nchini ambao ni:

  • Rose Mhando – anayejulikana kwa sauti yake ya kupenya na nyimbo zenye nguvu za kiroho

  • John Lissu – msanii mwenye uzoefu anayeleta ujumbe wa imani kupitia nyimbo zake

  • Vinance Malachi – mwanamuziki anayeendelea kujipatia umaarufu kwa nyimbo zake zenye kina cha kiroho

  • Agape Gospel Band – bendi inayojulikana kwa uchezaji bora na kusindikiza nyimbo za injili kwa ubora wa hali ya juu

  • Na wengine wengi watakaotangazwa

Maana ya Usiku wa Rehema

Usiku wa Rehema (International Night of Mercy – INOM) ni mkutano maalum wa maombi na sifa unaolenga kuwakutanisha waumini katika hali ya toba na kusihi rehema za Mungu. Katika muktadha wa Kikristo, hasa wakati wa kukumbuka mateso na kifo cha Yesu Kristo, wakati huu ni wa kutafakari upendo na rehema alizoonyesha kwa wanadamu.

Maandalizi na Mwaliko

Waandalizi wanatoa wito kwa wote kujitayarisha kiroho na kimwili kwa ajili ya usiku huu wa baraka.

"Usikose katika Usiku huu wa Rehema; USIKU WA REHEMA! JIANDAE!" – ndio kaulimbiu inayowavutia wengi kuhudhuria.



 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv