Tangazo hilo limetolewa jana Ijumaa Aprili 17, 2026 kupitia Gazeti la Serikali ambapo zitaanza kutumika siku 14 tangu kutangazwa rasmi kwa mujibu wa gazeti hilo.
Aidha, imeeleza kuwa marekebisho hayo yamefanywa kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, Sura ya 413, kinachoiruhusu LATRA kupanga na kurekebisha viwango vya nauli na tozo za huduma za usafiri.
Kwa mujibu wa jedwali lililotolewa, nauli za mabasi ya masafa marefu zimepangwa kulingana na daraja la basi na hali ya barabara. Kwa mabasi ya kawaida (ordinary), abiria atalipa Sh57.93 kwa kilometa moja katika barabara ya lami na Sh66.62 kwa barabara ya vumbi.
Kwa upande wa mabasi ya kati (semi-luxury), nauli kwa kilometa moja kwenye barabara ya lami ni Sh74.18. Pia, mabasi ya mijini (daladala), viwango vipya vinaonyesha kuwa safari ya hadi kilomita 10 itagharimu Sh700, huku nauli ikiongezeka kulingana na umbali hadi kufikia Sh1,500 kwa safari ya kilomita 36 hadi 40.


Post a Comment