Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Upendo wa Mtakatifu Francisco wa Asizi Mahenge, Sista Senorina Lukwachala Anatangaza kifo cha Sista Salome Simalike, Kilichotokea Tarehe 26.04.2026 usiku huko Ifakara alipokuwa akipatiwa Matibabu. Misa ya kumwombea na Kumuaga Marehemu Sista Salome Simalike, itaadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Andrea Mtume Kanisa Kuu, Jimbo Katokiki Ifakara Maziko yatafanyika siku ya Jumatano tarehe 29.04.2026, Saa 5 Asubuhi Utawani Itete, Jimbo Katoliki Mahenge Habari ziwafikie
Mhashamu Agapit Ndorobo, Askofu wa Jimbo Katoliki Mahenge Mhashamu Salutaris Libena, Askofu wa Jimbo Katoliki Ifakara. Mapadre wote wanaofanya utume Jimbo Katoliki Mahenge na Ifakara. Masista wote wa Shirika la Upendo wa Mtakatifu Francisko wa Asizi Mahenge. Wazazi, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote pale walipo. Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie. Apumzike Kwa amani. Amina.

Post a Comment