#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

Mchungaji Bilalo amuuwa mke wake

Mwanaume mmoja aitwaye Kasese Gerevas Bilalo (47), ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Habari Njema na Mkazi wa Kijiji cha Nyarututu, Kata ya Bwanga, Wilaya ya Chato mkoani Geita, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe, Martha Faustine (45), Mkazi wa Wilaya ya Chato Mkoani humo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, SACP Safia Jongo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji na kusema chanzo chake kinadaiwa kuwa ni migogoro ya kifamilia iliyotokana na marehemu kumtuhumu mumewe kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa, hali iliyosababisha migogoro ya mara kwa mara katika familia hiyo.
Kwa mujibu wa Kamanda SACP Jongo, tukio hilo limetokea Mei 12, 2026, majira ya saa sita mchana katika Kijiji cha Nyarututu, Kata ya Bwanga, Wilaya ya Chato, ambapo marehemu alikutwa amefariki dunia ndani ya nyumba yao katika mazingira ambayo Jeshi la Polisi limeeleza kuwa yalitengenezwa ili kuonekana tofauti na uhalisia.
Aidha, uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa alimvizia mkewe akiwa amelala, kisha akamkaba shingoni kwa kutumia kamba ya katani kabla ya kumning’iniza juu ya kenchi ili tukio hilo lionekane kama la kujinyonga.
Kamanda SACP Jongo amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa ajili ya uchunguzi zaidi, huku taratibu nyingine za kisheria zikiendelea kukamilishwa ili mtuhumiwa afikishwe kwenye mamlaka husika za kisheria.








Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv