Chelsea wamewauliza Inter Milan ikiwa watamjumuisha kiungo wa kati wa Italia Nicolo Barella, 26, katika makubaliano ya kubadilishana ambayo yatamfanya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, kuhamia Italia kwa mkataba wa kudumu. (Corriere dello Sport - in Italian)
Manchester United wanatayarisha dau la pauni milioni 45 kwa mlinda lango wa Everton Jordan Pickford, 29. (Star Sunday)
Newcastle wamemuongeza beki wa kushoto wa Chelsea Mhispania Marc Cucurella, 24, kwenye orodha ya walengwa inayotaka kuwasajili msimu wa joto. (Sunday Mirror)
Chelsea pia wanatazamia kumuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, winga wa Morocco Hakim Ziyech, 30, na kipa wa Senegal Edouard Mendy, 31, kwa klabu za Saudia. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Chelsea huenda ikamkabidhi kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 23, kwa Brighton kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili kiungo wa Ecuador Moises Caicedo, 21.. (Observer)
Liverpool na Chelsea wameulizia kuhusu kiungo wa kati wa Celta Vigo na Uhispania Gabri Veiga, 21 (Fabrizio Romano)
Al-Hilal wamekubali makubaliano ya kibinafsi na mlinzi wa Senegal Kalidou Koulibaly, 31, juu ya uwezekano wa kuhama kutoka Chelsea . (Ekrem Konur)
Paris St-Germain wamezungumza na meneja wa Arsenal Mikel Arteta kuhusu kuwa kocha wao mpya, huku mazungumzo yakiwa yamevunjika na kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann.(RMC Sport - in French)
Kipa wa Brentford ya Uhispania David Raya, 27, amekubali masharti ya kibinafsi na Tottenham . (Fabrizio Romano)
Liverpool wanavutiwa na kiungo wa kati wa Uholanzi Ryan Gravenberch, 21, ambaye ameeleza kutoridhika kwake na kukosa muda wa kucheza Bayern Munich msimu uliopita. (Bild - in German)
West Ham wameanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa kumpata beki wa Everton mwenye umri wa miaka 20 Muingereza Jarrad Branthwaite (Football Insider)
Real Betis pia wana nia ya kumsajili beki wa Manchester United raia wa Ivory Coast Eric Bailly, 29, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Marseille. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Juventus wameanza mazungumzo juu ya kumsajili Timothy Castagne kutoka Leicester City , ambaye wanataka euro 15m (£12.8m) kwa beki huyo wa pembeni wa Ubelgiji, 27. (Fabrizio Romano)
Real Betis wanataka kuafiki mkataba wa kudumu na fowadi wa Uhispania Ayoze Perez, 29, ambaye alijiunga kwa mkopo kutoka Leicester mwezi Januari. (AS - in Spanish)
Bayern Munich wanasema hawana nia ya kumuuza Joshua Kimmich na wakaikosoa Barcelona kwa 'kufanya mzaha' ili kumvutia kiungo huyo wa kati wa Ujerumani, 28. (Sky Sport Germany, via Goal)
Kocha wa Barcelona Xavi anavutiwa na mkataba ambao utamfanya kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie, 26, kujiunga na Inter Milan , huku kiungo wa kati wa Croatia Marcelo Brozovic, 30, akielekea upande mwingine.(Sport - in Spanish)
Baada ya kukatisha mkataba wake na Real Madrid , fowadi wa zamani wa Ubelgiji Eden Hazard, 32, anafikiria kurejea nyumbani kucheza pamoja na mdogo wake Kylian katika klabu ya RWD Molenbeek .(Sacha Tavolieri)
Jordi Alba amekubali mkataba na Inter Miami baada ya kuondoka Barcelona lakini beki huyo wa pembeni wa Uhispania, 34, bado ana ofa kutoka kwa Atletico Madrid , Inter Milan na ligi ya Saudia. (Mundo Deportivo - in Spanish)





Post a Comment