Mamlaka ya Uganda imesema kuwa imewakamata watu watatu kuhusiana na shambulizi dhidi ya shule siku ya Ijumaa ambapo takriban watu 40 waliuawa.
Wengi wa waathiriwa walikuwa wanafunzi wa shule ya Lhubiria iliyoko katika mji wa Magharibi wa Mpondwe.
Wengi walichomwa hadi kufa katika bweni lao.
Mkuu wa Wilaya Joe Walusimbi alisema kukamatwa kwa watu hao kumefuatia vidokezo kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.
Lakini aliongeza kuwa jeshi la Uganda bado lilikuwa likiwasaka wanamgambo hao wa Kiislamu ambao wamekuwa wakilaumiwa kwa shambulio hilo na wanaripotiwa kukimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Post a Comment