Leo Jumatatu Juni 19, 2023 amehitimisha ushahidi wake aliouanza Ijumaa iliyopita, baada ya kuhojiwa maswali ya dodoso kutoka kwa mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, Peter Kibatala na Nehemia Nkoko, kuhusiana na ushahid wake mkuu alioutoa wakati akiongozwa na mwendesha mashtaka.
Hata hivyo katika mahojiano hayo, shahidi huyo Kachero mwenye cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), alikuwa na majibu ya kufikirisha baada ya kujibu maswali mengi kuwa hakumbuki taratibu zinazomuongoza kutekeleza majukumu yake ndani ya jeshi hilo wala nyenzo za kazi zikiwemo nyaraka muhimu.
Post a Comment