Manowari inayotumika kuwasafirisha watalii kutazama ajali ya meli ya Titanic imepotea katika bahari ya Atlantiki, na hivyo kusababisha kazi ya utafutaji na uokoaji
Mlinzi wa Boston Coastguard aliiambia BBC kuwa operesheni ya kutafuta meli hiyo ilikuwa ikiendelea Jumatatu.
Haijabainika ni watu wangapi, ikiwa wapo, walikuwa kwenye meli hiyo ilipotoweka.
Manowari ndogo mara kwa mara husafirisha watalii wanaolipa ili kutazama ajali ya Titanic.
Meli hiyo ipo koina cha mita 3,800 (12,500ft) chini chini ya sakafu ya bahari ya Atlantiki. Ni takriban 600km (maili 370) kutoka pwani ya Newfoundland, Canada.
Meli hiyo ya abiria, ambayo ilikuwa meli kubwa zaidi wakati wake, iligonga jiwe la barafu katika safari yake ya kwanza kutoka Southampton hadi New York mwaka wa 1912. Kati ya abiria 2,200 na wafanyakazi waliokuwa ndani, zaidi ya 1,500 walikufa.
Meli ya Titanic imeimetazamwa sana tangu ajali hiyo ilipogunduliwa mwaka wa 1985.
Post a Comment