Chelsea imefanya mawasiliano na Ajax kuhusu nia yao ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus, 22. (The Athletic)
Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Victor Osimhen na timu yake ya Napoli bado yamekwama, na hivyo kufungua milango kwa Chelsea au Manchester United kujaribu kumsajili mshambuliaji huyo wa Nigeria, 24. (Corriere dello Sport, via Goal).
Inter Milan wanaamini kuwa sasa haiwezekani kufikiria kumrejesha Romelu Lukaku katika klabu hiyo kutoka Chelsea baada ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, 30, kuwasiliana na wapinzani wao AC Milan na Juventus kuhusu uwezekano wa kuhamia huko. (Gazzetta dello Sport)

Post a Comment