#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

Waganga wafawidhi kusimamia majukumu Yao Wilaya ya Meru

 Mkuu wa idara ya Afya,Lishe na Ustawi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Evarist Chiweka ameongoza kikao kazi cha Waganga wafawidhi na waratibu wa Afya ngazi ya Halmashauri kujadili Taarifa ya utekelezaji Robo ya pili ya Mwaka 2024-2025. 

 Aidha Dkt. Chiweka katika kikao hiko amewataka Waganga wafawidhi kusimamia majukumu Yao hasa katika kuhakikisha Wananchi wanapata huduma kama inavyostahili Kwa kutumia taaluma zao na namna walivyo aminika na Serikali. 



Aidha amesisitiza swala la kuendelea kutoa Elimu Kwa Jamii kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya na kutoa Elimu na hamasa Kwa wakina Mama wajawazito kuanza kliniki mapema ili kuepusha matatizo wakati wakujifungua na matatizo Kwa Mtoto alie tumboni.

Kikao hiko kimeuzuriwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ambae amewataka Waganga hao kusimamia vizuri swala la Mapato kwani Mapato yanapokuwa mazuri itasaidia utoaji wa huduma Bora kwenye Vituo wanavyofanyia kazi, nakusisitiza swala la nidhamu mahali pakazi kama nyenzo Imara ya kudumisha upendo katika Maeneo ya Kazi na kusaidia kuleta tija Kwa Wananchi tunao wauhudumia





Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv