Katika kuendeleza juhudi za raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Neema Lugangira ameweza kukutana na viongozi wote vyama vya siasa wilayani Arumeru.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook qmeandika "Nimekutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani Arumeru kutoka CCK, DP, CHAUMMA, SAU, ADA TADEA, UPDP, UMD, CUF, NRA, Demokrasia Makini, ACT Wazalendo, AAFP, UDP, TLP, CHADEMA na NLD.
Tumekubaliana kushirikiana kwa maendeleo ya wananchi, kwa kuzingatia falsafa ya 4R za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tofauti za kisiasa hazitatutenganisha katika kuleta maendeleo.
#ArumeruKimataifa #AmaniArumeru #MaendeleoArumeru #TukutaneSite
Post a Comment