#-----------Start surfernetwork.com--------------- # Ads.txt last updated on:  2026/06/10 13:26:00.23423 by surfernetwork.com MANAGERDOMAIN=surfernetwork.com CONTACT=support@surfernetwork.com # SurferNETWORK surfernetwork.com, 204, DIRECT # Adswizz adswizz.com, 724, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 #Azerion targetspot.com, 455, RESELLER, feb28ed826dcf532 improvedigital.com, 2734, RESELLER adswizz.com, 172, RESELLER, 52ded3ee71b94c84 appnexus.com, 7265, RESELLER, f5ab79cb980f11d1 tritondigital.com, 44733, RESELLER, 19b4454d0b87b58b rubiconproject.com, 9753, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #US rubiconproject.com, 16418, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #EMEA # DAX thisisdax.com, 5460, RESELLER thisisdax.com, 5461, RESELLER # katz Katzdigital.com, 318, RESELLER Katzdigital.com, 80, RESELLER # Magnite rubiconproject.com, 8441, RESELLER, 0bfd66d529a55807 #-----------End surfernetwork.com-----------------

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na mke wake Mama Salma Kikwete ameitembelea jamii ya Wahadzabe wanaoishi katika Kijiji cha Endamagha kilichopo Kata Tarafa ya Eyasi, Wilaya ya Karatu.

Katika ziara yao hiyo Dkt. Kikwete na mkewe wamepata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ya mila na desturi za jamii hiyo ya Wahadzabe hususan njia zao za asili za kutafuta na kuhifadhi vyakula, malezi ya watoto, makazi yao, nk. 

Pamoja na mambo mengine  waliweza pia kuongea kwa kina na wanajamii hao kuhusu changamoto zinazowakabili kama vile changamoto ya upatikanaji wa elimu kutokana na mfumo wao wa maisha wa kuhamahama, uvamizi wa makabila mengine katila maeneo yao ya asili hali inayotishia mtindo wao wa maisha pamoja na upatikanaji wa huduma nyingine muhimu za kijamii. 

Dkt. Kikwete alitumia fursa hiyo kuwapongeza wenyeji wake kwa kuendelea kudumisha mila na desturi zao huku wakitambua na kuzingatia umuhimu wa kuwapeleka watoto wao shule ili kupata elimu itakayokuja kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye. Aidha, aliwataka viongozi wa Serikali walioambatana naye kuzidisja ukaribu na jamii hiyo ili kusikiliza, kuzielewa na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za kipekee zinazoikabili jamii hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Mobile Logo Settings

Usa River Tv