Usa River Media kupitia Usa River Radio na Usa River TV inatangaza kuzindua vipindi maalum vya michezo vitakavyolenga michezo isiyokuwa soka. Vipindi hivi vitapatikana pia kupitia Usa River Blogspot kwa makala, matokeo, na mahojiano.
Lengo ni kuipa nafasi michezo kama netiboli, basketball, riadha, volleyball na mingineyo ambayo mara nyingi haiangaziwi vya kutosha na vyombo vya habari nchini Tanzania.
Kipindi hiki kitakuwa na sehemu za:
· Matokeo na ratiba ya michuano
· Mahojiano na wanamichezo na makocha
· Uchambuzi wa michezo
· Highlights za mechi
· Makala za kina kwenye blogu
Tunaamini Tanzania ina vipaji vingi zaidi ya soka. Kwa kushirikiana na shule, vyuo, na mashirikisho, tutawaletea mashabiki maudhui bora na ya kuelimisha.
Fuatilia Usa River Radio, Usa River TV, na Usa River Blogspot kila wiki kwa vipindi vipya vya michezo.
Post a Comment